Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: sambamba na kuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, takwimu zinaonyesha kuwa nusu ya familia za Waislamu nchini Uingereza wanahitaji msaada wa benki za chakula ili kupata futari yao ya siku.
Takwimu hizo za kutisha zilizofichuliwa Ijumaa iliyopita na taasisi moja ya Kiislamu ya masuala ya kibinadamu zinaonyesha kuwa, nusu ya familia za Waislamu nchini Uingereza mwaka huu hazina fedha za kuweza kukidhi mahitaji yao kwa ajili ya kununua futari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Taasisi ya Islamic Aid ya nchini humo imekadiria kuwa, nusu ya familia za Waislamu huko Uingereza zinaishi katika hali ya umaskini, kwa maana kwamba karibu Waislamu milioni moja na laki sita wanaishi katika hali ya umaskini ambao ni sawa na asilimia 18 ya jamii nzima ya wananchi wa Uingereza.
Wakati huo huo benki za chakula nchini humo ziko chini ya mashinikizo makubwa na maombi mengi ya wananchi wanaohitaji misaada sambamba na kuongezeka idadi ya Waislamu wanaoshi katika hali ya umaskini.
Nina Parmar mwakilishi wa benki ya chakula ya Sofreh huko Uingereza anasema: Familia za Waislamu zinakabiliwa na matatizo makubwa kutokana na matatizo ya kifedha na hivyo zinashindwa kulipa madeni na kukodi nyumba na gharama za za maisha.
Hali hii imekuwa ikiziathiri zaidi familia ambazo zina watoto zaidi ya wawili ambazo aghalabu ni familia za Waislamu. Familia hizo zinaishi katika nyumba zisizofaa huku zikiwa hazinufaiki kivyovyote na misaada ya kijamii kutokana na siasa zisizo za kiadilifu za serikali ya Uingereza.
342/